Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:44

Israel yatoa kanda ya video ikionyesha wapiganaji wakiwa ndani ya eneo la UN


Picha ya Video iliyochukuliwa na droni ikionyesha wapiganaji wakiwa ndani ya eneo la UN.
Picha ya Video iliyochukuliwa na droni ikionyesha wapiganaji wakiwa ndani ya eneo la UN.

Jeshi la Israel Jumanne (Mei 14) lilitoa kanda ya video iliyochukuliwa na droni ikiwaonyesha watu wenye silaha wakiwa wamesimama pembeni ya gari lililokuwa na nembo ya UN katika eneo la Umoja wa Mataifa huko kusini mwa Gaza, katika mji wa Rafah, na wameutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na IDF ilisema kuwa siku ya Jumamosi (Mei 11), wanajeshi walikuwa wamewatambua wapiganaji katika viwanja vya ghala kuu ya shirika la misaada la UN linalo wahudumia Wapalestina (UNRWA) mashariki mwa Rafah, ambako jeshi la Israeli limekuwa likifanya operesheni ya kijeshi kwa zaidi ya wiki moja.

Msemaji wa UNRWA alisema shirika hilo linaichunguza kanda hiyo ya video na watatoa taarifa mara itakapokuwa iko tayari.

Reuters iliweza kuifuatilia kanda hiyo ya video iliyochukuliwa karibu na majengo hayo, mlingoti, vyuma, matenki kwenye paa na majani yanafanana na picha ya satellite na picha nyingine zilizoko katika mafaili yao. Reuters haikuweza kuthibitisha kutoka vyanzo huru tarehe ambayo picha hiyo ilikuwa imechukuliwa.

UNRWA imekuwa ikilengwa kwa ukosoaji mkali wa Israel, ikilishutumu shirika hilo kwa kushirikiana na harakati za Kiislam za Hamas huko Gaza na imetaka ivunjwe.

Shirika hilo, lililokuwa limeanzishwa kuwasaidia wakimbizi wa Palestina waliokoseshwa makazi wakati wa vita ambavyo vilianza kipindi ambacho taifa la Israel lilianzishwa mwaka 1948, limekuwa likikanusha vikali tuhuma hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG