Maafisa wa kijeshi wanaotawala katika taifa hilo la Afrika Magharibi waliiambia Marekani kuondoa wanajeshi wake 1,000 nchini humo, nchi ambayo hadi mapinduzi ya mwaka jana ilikuwa mshirika mkuu wa Washington katika vita dhidi ya waasi ambao waliua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi mamilioni wengine.
Afisa mkuu wa jeshi la Marekani ambaye alizungumza katika msingi wa kutotajwa jina, amesema wanajeshi wa Russia hawakuwekwa pamoja na wanajeshi wa Marekani, lakini walitumia eneo tofauti la kambi ya jeshi la anga namba 101, iliyo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Diori Hamani mjini Niamey, mji mkuu wa Niger.
Hatua ya jeshi la Russia iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na Reuters, inawaweka wanajeshi wa Marekani na Russia kwenye sehemu moja iliyo karibu sana, wakati ambapo ushindani wa kijeshi na kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili unazidi kuongezeka kutokana na vita vya Ukaine.
“Hali sio nzuri lakini kwa muda mfupi inaweza kudhibitiwa,’’ afisa huyo alisema.
Forum