Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:10

Wafilipino watangaza 'usindi mkubwa' kwa kufikisha mahitaji kwa wavuvi Bahari ya South China licha ya vipingamizi


Eneo lenye mvutano baina ya Ufilipino na China la Scarborough Shoal huko katika Bahari ya South China.
Eneo lenye mvutano baina ya Ufilipino na China la Scarborough Shoal huko katika Bahari ya South China.

Kikundi cha Wafilipino kinachoongoza juhudi ya kusambaza mahitaji muhimu katika Bahari ya South China kimefikisha chakula na mafuta kwa wavuvi wa Ufilipino licha ya kufuatiliwa na vyombo vya majini vya China, maafisa wake walisema Alhamisi, wakiita ni “ushindi mkubwa.”

Atin Ito (Hii ni Yetu) alisema timu ya watu 10 walisafiri kwa boti hadi eneo la Scarborough Shoal siku moja kabla ya msafara wa kiraia, uliokuwa na boti tano za biashara na boti ndogo 100 za uvuvi zilianza safari zao.

“Juhudi hiyo ilifanikisha ushindi mkubwa wakati timu yake ya awali ilipowasili eneo karibu na Panatag Shoal Mei 15 (na) iliweza kugawanya mahitaji kwa wavuvi waliokuwa katika eneo hilo,” alisema Emman Hizon, msemaji wa Atin Ito, akitumia jina la kienyeji la Scarborough.

Eneo hilo lilioko ndani ya maili 200 ya eneo la baharini la Manila (kilomita 370) eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, Scarborough Shoal inamvuto kutokana na wingi wa samaki wake na aina ya miti ya samawati ambayo hutoa hifadhi kwa vyombo vya baharini bahari inapochafuka.

Eneo ambalo China inalidhibiti na ambalo inaliita Kisiwa cha Huangyan ambalo Ufilipino na nchi nyingine inalitambua kama ni Scarborough Shoal.
Eneo ambalo China inalidhibiti na ambalo inaliita Kisiwa cha Huangyan ambalo Ufilipino na nchi nyingine inalitambua kama ni Scarborough Shoal.

China ilisema Jumatano ina mamlaka juu ya eneo la Shoal, ambacho inakiita Kisiwa cha Huangyan, pamoja na eneo la majini lilioko karibu. Televisheni ya serikali ya China CCTV ilisema walinzi wa pwani wa China walifanya “shughuli za kawaida za haki ya kulinda eneo na kuhakikisha sheria inafuatwa” katika eneo la majini linalozunguka Shoal siku ya Jumatano.

Hizon aliiambia Reuters kwamba timu iliyokuwa imetangulia ilikuwa ni sehemu ya mpango wa dharura wa kikundi hicho iwapo China ingezuia msafara mkuu wa vyombo hivyo vya baharini, ambayo alisema utarejea katika bandari ya Ufilipino Alhamisi baada ya kusafiri hadi katika eneo la majini la umbali wa maili 50 kutoka Shoal.

Hizon alisema msafara mkuu haukuhitajika kwa sababu wavuvi, tayari walikuwa wamefikishiwa mahitaji na meli zilizotangulia, na waliondoka eneo hilo baada ya vyombo vya baharini vya China kuwalazimisha kuondoka eneo hilo.

Ndege ya Walinzi wa Pwani wa Ufilipino (PCG) iliyoko katika eneo kwa ajili ya kufuatilia hali ya Scarborough Shoal Jumatano ilishuhudia vyombo vya baharini vya China 19, ikiwemo manowari moja ya China, katika eneo. PCG ilisema pia inafuatilia vizuizi viwili vinavyoelea vilivyopo kusini mashariki mwa lango la kuingia Shoal.

Forum

XS
SM
MD
LG