Kupitia ujumbe wa X, msemaji wa walinzi wa pwani wa Ufilipino Jay Tarriela, amesema kwamba meli ya China iliendeshwa kwa njia ya hatari dhidi ya meli mbili za walinzi wa pwani wa Ufilipino, na hivyo kusababisha uharibifu mdogo kwenye moja ya meli hizo.
Ujumbe tofauti uliotolewa na kikosi cha Ufilipino kwenye bahari ya South China Sea umesema mabaharia wanne kwenye meli ya pili waliumia baada ya kushambuliwa na bomba la maji kutoka kwenye meli ya China.
Meli zote mbili za Ufilipino zilikuwa zinasindikiza meli mbili za mizigo, pamoja na kikosi kipya cha wanajeshi kuelekea kwenye meli ya kijeshi ya Ufilipino iliyopo kwenye eneo la bahari hiyo la Second Thomas Shoal, ikilinda eneo la bahari la taifa hilo.
Walinzi wa pwani wa China wametoa taarifa wakilaumu meli za Ufilipino kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la China Renal.
Forum