Jeshi la anga la Ufilipino limesema Jumatano kwamba ndege yake ya kivita imeshiriki katika doria ya pamoja Jumanne, huko Batanes, ambalo ni jimbo la kaskazini mwa Ufilipino lililopo takriban kilomita 200 kutoka Taiwan, kisiwa kinachojitwala, ambacho China inadai kuwa himaya yake.
Zoezi hilo linaendelea hadi Alhamisi, likishirikisha wanajeshi wa majini wa Marekani na Ufilipino. Zoezi hilo limekuja siku chache tu baada ya rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, kusema kwamba hali ni tete kwenye bahari hiyo, wakati China ikijaribu kusimika ushawishi wake, kwenye eneo hilo ambalo linazozaniwa na mataifa ya kieneo.
China imekuwa ikidai kumiliki maji yote ya South China Sea, suala ambalo limepelekea mzozo kati yake na Ufilipino, Vietnam, Malaysia, Taiwan na Brunei.
Forum