Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:29

ASEAN yataka utulivu katika bahari ya South China


Wanachama wa jumuiya ya mataifa 10 ya kusini mashariki mwa Asia, (ASEAN), pamoja na Australia wanahimiza utulivu kati ya wale wanaoendesha shughuli zao ambazo zinaanza kuwa tete katika bahari ya South China.

Ombi hilo limetolewa Jumatano katika taarifa ya pamoja kati ya mataifa ya ASEAN na Australia mwishoni mwa mkutano wa siku tatu jijini Melbourne. Mkutano huo uliadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 ya Australia kuanzisha uhusiano rasmi na ASEAN.

Tamko hilo limesema Australia na ASEAN zinatambua faida za kuwa na bahari ya South China, iliyo tulivu na yenye ustawi, ambapo imehimizwa kwa nchi zote kuepuka hatua zozote za upande mmoja ambazo zinaweza kutishia matamanio hayo.

Lakini taarifa hiyo haikujumuisha matamshi ambayo yameitaja China moja kwa moja kuwa na makabiliano mengi na mataifa mengine katika eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG