Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:07

Rais wa Ureno asema kuna haja nchi yake ilipe fidia kwa waathirika wa utumwa


Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Soussa
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Soussa

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Soussa Jumanne alisema nchi yake iliwajibika kwa uhalifu uliofanywa wakati wa enzi ya utumwa na ukoloni, na amesema kuna haja ya kulipa fidia.

Kwa zaidi ya karne nne, takriban Waafrika milioni 12.5 walitekwa nyara, na kusafirishwa kwa nguvu umbali mrefu na meli za Ulaya na wafanya biashara wa magendo na kuuzwa kama watumwa.

Wale walionurusika katika safari hiyo waliishia kutumikishwa kwenye mashamba ya kanda ya Amerika, hasa Brazil na nchi za Caribbean, huku wengine wakinufaika na kazi hiyo.

Portugal ilisafirisha kwa njia haramu karibu Waafrika milioni 6 kuliko taifa lingine lolote la Ulaya, lakini kufikia sasa imeshindwa kukabiliana na historia yake na ni machache sana yanayofundishwa shuleni kuhusu jukumu lake katika utumwa.

Akizungumza katika hafla na waandishi wa habari wa kigeni Jumanne, Rebelo de Soussa alisema Ureno “inawajibika kikamilifu” kwa makosa ya miaka ya nyuma na kwamba uhalifu huo, ikiwemo mauaji ya enzi ya ukoloni yalikuwa na madhara.

“Lazima tulipe fidia kwa madhara hayo,” alisema.

Je kuna vitendo ambavyo havikuadhibiwa na waliohusika hawakukamatwa? Je kuna bidhaa zilizoporwa na hazikurudishwa? Tutizame jinsi ya kurekebisha hali hii, aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG