Mpiganaji huyo, Anywari Al Iraq, raia wa Uganda, alikamatwa katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako kundi la waasi la Allied Democratic Forces lina makao yake, jeshi la Uganda People's Defense Forces, lilisema katika taarifa yake.
Wakati wa operesheni hiyo, watu tisa wakiwemo watoto, waliokolewa kutoka eneo la jimbo la Ituri, mashariki mwa Kongo, kwa mujibu wa jeshi hilo.
"Aina ya vifaa vya kutengenezea vilipuzi vilivyoboreshwa (IED) vilipatikana," ilisema.
Waasi wa ADF walianzia nchini Uganda lakini wamejikita nchini Kongo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990. Kundi hilo liliahidi utiifu kwa Islamic State, katikati ya mwaka 2019 na linashutumiwa kuwaua mamia ya wanakijiji katika uvamizi wa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.
Forum