Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:18

Viongozi wa dunia wampongeza Claudia Sheinbaum, rais wa kwanza mwanamke wa Mexico


Rais mteule wa Mexico Claudia Sheinbaum
Rais mteule wa Mexico Claudia Sheinbaum

Claudia Sheinbaum alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi nchini Mexico na kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo, akirithi mradi wa mshauri wake na kiongozi anayeondoka madarakani Andres Manuel Lopez Obrador ambaye hatua zake maarufu za kupambana na umaskini zilimsaidia kupata ushindi.

Viongozi kadhaa wa dunia walimpongeza baada ya ushindi huo wa kihistoria.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema “ Ninampongeza Claudia Sheinbaum kwa uchaguzi wake wa kihistoria kama Rais wa kwanza mwanamke wa Mexico. Natarajia kufanya kazi kwa karibu na Rais mteule Sheinbaum kwa nia ya ushirikiano na urafiki unaozingatia uhusiano wa kudumu kati ya nchi zetu mbili.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula Da Siliva alisema “ Nimefurahishwa sana na ushindi wa Sheinbaum, mwanamke mwenye sera za maendeleo anayeongoza Mexico, ushindi wa demokrasia, na pia kwa rafiki yangu Lopez Obrador, ambaye aliongoza serikali isiyo ya kawaida.”

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema “Natarajia kufanya kazi kwa karibu na Rais mteule Sheinbaum kuimarisha zaidi urafiki kati ya Canada na Mexico, ambao umejikita katika uhusiano wa kitamaduni, vipaumbele vya pamoja, na uhusiano wa kibiashara na uwekezaji.

Forum

XS
SM
MD
LG