Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 14:07

Baraza la Wawakilishi la Marekani lapitisha mswada unaoweka vikwazo kwa waendesha mashtaka wa ICC


Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan

Baraza la Wawakilishi la Marekani linaongozwa na Warepublican Jumanne limepitisha mswada ambao utaiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa uamuzi wa Mwendesha mashtaka wake mkuu kutaka zitolewe hati za kimataifa za kuwakamata maafisa wa Israel wanaohusishwa na vita huko Gaza.

Mswada huo umepigiwa kura 247 dhidi ya 155, huku Wademocrats 42 wakijiunga na Warepublican kuunga mkono mswada huo.

Mswada huo hautarajiwi kuwa sheria, lakini unadhihirisha uungwaji mkono wa Israel unaoendelea katika Baraza la Wawakilishi licha ya ukosoaji wa Jumuia ya Kimataifa kwa jinsi nchi hiyo ya Mashariki ya Kati inavyoendesha vita katika Ukanda wa Gaza.

Ikulu ya Marekani mwezi uliopita ilikosoa uamuzi wa ICC kutaka hati hizo zitolewe.

Mswada huo hautarajiwi kuwasilishwa katika Baraza la Seneti linalodhibitiwa kwa idadi ndogo na Wademocrats ili upigiwe kura.

Mswada huo unanuia kuwawekea vikwazo watu wanaohusika kwa kuwafangulia mashtaka Wamarekani au raia wa nchi shirika za Marekani ambazo sio wanachama wa ICC, ikiwemo Israel.

Kama ungekuwa sheria, mswada huo pia ungewazuia maafisa wa ICC kuingia Marekani, na kufuta viza yoyote ya Marekani na kuwazuia kununua au kumiliki mali nchini Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG