Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 03:01

IMF yaidhinisha mkopo wa dola milioni 570 kwa Zambia


Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva akizungumza na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema wakati wa mkutano Ikulu mjini Lusaka, Januari 23,2023. Picha ya AP
Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva akizungumza na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema wakati wa mkutano Ikulu mjini Lusaka, Januari 23,2023. Picha ya AP

Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Jumatano limesema bodi yake ya utendaji imekamilisha tathmini ya tatu ya mpango wa kuirahisishia Zambia kuendelea kupata mikopo na imeidhinisha mkopo wa mara moja wa dola milioni 569.6.

Bodi hiyo imeidhinisha pia ombi la Zambia la kuiongezea msaada wa kifedha kutoka dola bilioni 1.3 hadi dola bilioni 1.7 ili kulisaidia taifa hilo la Kusini mwa Afrika kukabiliana na ukame mbaya, ambao ulisababisha hasara upande wa mazao na kuathiri uzalishaji wa umeme.

Katika taarifa, afisa wa IMF Antoinette Sayeh amesema mamlaka za Zambia zilipiga hatua ya kuridhisha kuhusu mageuzi ya kiuchumi na kimkakati, huku zikikabiliana na changamoto za kibinadamu kutokana na ukame.

“Kuendelea mbele, kuratibu sera za uchumi, juhudi zinazoendelea za kurejesha ustahimilivu wa fedha na madeni, na utekelezaji wa mageuzi thabiti utakuwa muhimu katika kukabiliana na athari za ukame, kudumisha uthabiti wa uchumi, na kuimarisha ukuaji,” amesema Sayeh, naibu mkurugenzi wa IMF.

Zambia yenye utajiri wa shaba ilijikwamua kutoka kwenye tatizo la kushindwa kulipa madeni mwezi huu baada ya mchakato wa kurekebisha deni ambao ulichukua zaidi ya miaka mitatu na nusu na ilikuwa tahadhari kwa utaratibu wa mfumo wa pamoja wa kundi la G20 ulioundwa kusaidia nchi za kipato cha chini kukabiliana na mzigo wa madeni makubwa.

Waziri wa fedha wa Zambia wiki iliopita aliliomba bunge kupitisha matumizi ya ziada ya dola bilioni 1.65 kusaidia kulipa deni la nje na kukabiliana na ukame.

Forum

XS
SM
MD
LG