Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:28

Waasi wa Kihouthi wa Yemen washambulia meli mbili za biashara na meli ya kivita ya Marekani


Meli ya biashara iliyoshambuliwa na waasi wa Houthi wa Yemen katika Ghuba ya Aden, Januari 17, 2024.
Meli ya biashara iliyoshambuliwa na waasi wa Houthi wa Yemen katika Ghuba ya Aden, Januari 17, 2024.

Waasi wa Kihouthi wa Yemen Jumapili walisema walishambulia meli mbili za kiraia, na moja ya kivita ya Marekani katika Bahari ya Sham na Bahari ya Arabia, katika juhudi zao za hivi karibuni kuzorotesha safari za meli katika kile wanachosema ni kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.

Katika taarifa, msemaji wa jeshi la Wahouthi, Yahya Saree, alisema kundi hilo la kijeshi lilifyatua makombora dhidi ya meli ya kivita ya Marekani, makombora mawili ya kulenga meli dhidi ya meli iitwayo Captain Paris, na kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya meli iitwayo Happy Condor.

Mapema Jumapili, Mamlaka ya Uingereza ya operesheni za usafirishaji wa biashara baharini (UKMTO) ilisema kwamba meli iliyokuwa umbali wa maili 40 kusini mwa al Mukha huko Yemen iliripoti milipuko miwili karibu na eneo hilo.

Meli hiyo pamoja na wahudumu wake wako salama na wameendelea na safari yao, mamlaka hiyo ilisema bila kuitambulisha meli hiyo.

Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran, ambao wanadhibiti mji mkuu wa Yemen na maeneo mengi yenye watu wengi, walifanya mashambulizi kadhaa dhidi ya meli za kimataifa katika Bahari ya Sham tangu mwezi Novemba kwa mshikamano na Wapalestina.

Forum

XS
SM
MD
LG