Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:17

Mpaka kati ya Libya na Tunisia wafunguliwa tena


Lori likiingia Tunisia kutoka Libya kwenye mpaka wa Ras jedir uliofunguliwa Jumatatu.Picha ya maktaba
Lori likiingia Tunisia kutoka Libya kwenye mpaka wa Ras jedir uliofunguliwa Jumatatu.Picha ya maktaba

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Libya mjini Tripoli amesema kuwa mpaka muhimu na Tunisia wa Ras Ijdir umefunguliwa Jumatatu, miezi mitatu baada ya kufungwa kutokana na mapambano ya  silaha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baada ya hali ya utulivu kurejea, mpaka huo ulifunguliwa kwa kiasi, kati kati mwa Juni, kwa ajili ya upelekaji wa huduma za kibinadamu pamoja na kesi za kimatibabu, pamoja na zenye vibali maalum kutoka kwa wizara za usalama za Tunisia na Algeria.

Magari kadhaa ya dharura ya kubeba wagonjwa kutoka Libya yameonekana yakiingia Tunisia wakati wa ufunguzi huo uliohudhuriwa na waziri wa usalama wa ndani wa serikali ya Umoja wa Kitaifa yenye makao yake Tripoli, Emad Trabulsi, na mwenzake wa Tunisia, Khaled Nouri.

“ Saa mbili baada ya hafla hii, watu wa Libya wataweza kuingia Tunisia,” Trabulsi ameambia wanahabari, akiongeza kuwa mpaka huo umefunguliwa kwa ajili ya shughuli zote isipokuwa ulanguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG