Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:10

Putin na Kim Jong Un wakubaliana kuimarisha uhusiano wa mataifa yao


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akimkaribisha Rais Vladimir Putin alipowasili mjini Pyongyang, Juni 19, 2024.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akimkaribisha Rais Vladimir Putin alipowasili mjini Pyongyang, Juni 19, 2024.

Rais wa Russia Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekubaliana kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao, wakati wa mkutano wao katika siku ya kwanza ya ziara ya Putin mjini Pyongyang Jumatano, vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimesema.

Putin alifanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita akiahidi kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiusalama na taifa hilo lililotengwa lenye silaha za nyuklia na kuliunga mkono dhidi ya Marekani.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili unaonyesha “kutoshindwa na kudumu” kwa urafiki kati ya Korea Kaskazini na Russia, kulingana na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini(KCNA).

Uhusiano wa Korea Kaskazini na Russia umeimarika “kama ngome imara ya kimkakati kwa kulinda sheria ya kimataifa, amani na usalama na kichocheo kwa kuharakakisha ujenzi wa ulimwengu wenye misimamo tofauti,” KCNA limesema.

Maafisa mjini Washington na Seoul wanasema Korea Kaskazini iliipa silaha Russia kuisaidia katika vita nchini Ukraine.

Moscow na Pyongyang zilikanusha kupeyana silaha lakini zimeapa kuimarisha uhusiano wa kijeshi yakiwemo mazoezi ya pamoja kijeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG