Radio
06:00 - 06:30
Wanasayansi na maafisa wa serikali Kenya wahitilafiana kuhusu vyakula vya GMO
Tofauti kali zimeibuka nchini Kenya baada ya baraza la mawaziri Jumatatu kuondoa marufuku iliyokuwepo kwa miaka 10 ya vyakula na mazao yaliyokuwa kwa njia ya kibioteknolojia huku wakosoaji wa hatua hiyo wakisema ni hatari mno kwa afya ya wananchi.
19:30 - 19:59
Kenya: Mvutano kuhusu nani kiongozi halisi wa walio wengi Bungeni
Mzozo unaozingira swala la ni nani kiongozi halisi wa walio wengi katika bunge la Kenya, umemlazimu Spika wa bunge hilo Moses Wetangula kumteua Naibu Spika Gladys Boss kwa muda mfupi, kusimamia kamati ya kuratibu shughuli za bunge ili kusitisha usambaratishaji wa shughuli za taasisi hiyo.
21:00 - 21:29
Kwa Undani: Korea kaskazini imeendelea kufyatua makombora ya masafa marefu licha ya onyo kutoka kwa Marekani, Japan na Korea kusini
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.