Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:46

Kampuni ya Airbus yasema itachukuwa muda usafiri wa anga kuimarika


Ndege ya Lufthansa airbus ikiwa uwanja wa ndege wa Frankfurt, Ujerumani, Jumatatu, Aprili 20, 2020. Kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona asilimia 97 ya safari za ndege za Lufthansa zilisimamishwa (AP Photo/Michael Probst)
Ndege ya Lufthansa airbus ikiwa uwanja wa ndege wa Frankfurt, Ujerumani, Jumatatu, Aprili 20, 2020. Kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona asilimia 97 ya safari za ndege za Lufthansa zilisimamishwa (AP Photo/Michael Probst)

Kampuni ya ndege Ulaya Airbus imesema Jumatano sekta ya usafiri wa anga iko katika mgogoro mkubwa kutokana na janga la virusi vya corona na itachukuwa muda kuweza kujenga imani ya watu kutumia usafiri wa ndege.

Usafiri wa ndege umepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na mkusanyiko wa katazo la kusafiri na watu kuamua kubakia nyumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Airbus

Kampuni ya Airbus imetangaza matokeo ya robo ya kwanza ya biashara yake, ikisema imepoteza dola za Marekani milioni 522 wakati ikiwasimamisha kazi maelfu ya wafanyakazi na kuweza kuuza ndege chache zaidi 40 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka 2019.

Ujerumani

Viwanda ni sekta nyingine ambayo serikali nyingi zinaangalia wakati zikianza kuondoa masharti ya kibiashara ili kuwarudisha watu makazini na kuanza tena shughuli za kiuchumi zilizokuwa zimesimama.

Kampuni za magari kadhaa Ujerumani zimeanza tena uzalishaji lakini kwa kuweka masharti ya wafanyakazi kutokukaribiana.

Nchi hiyo imeanza kuondoa baadhi ya masharti mengine ya dharura yaliyowekwa katika amri ya kutotoka nje, ikiwemo kufungua maduka, lakini kuanzia Jumatano watu wanalazimika kuvaa maski usoni kuingia madukani.

“Sote inatulazimu kuwa waangalifu kwamba hili la kurejea kwa shughuli za uchumi halipelekei kuwa na maambukizi zaidi,” amesema Lothar Wieler, rais wa Taasisi ya Berlin Robert Koch.

Korea Kusini

Korea Kusini inawataka watu kuvaa maski wanaposafiri kwa likizo ndefu wikiendi ili kuendeleza yale yaliyofikiwa nchini katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Maafisa wa afya wameripoti maambukizi mapya tisa nchini Korea Kusini Jumatano, imefanya idadi ya waliopimwa na kuthibitishwa kuwa na maambukizi kufikia jumla ya watu 10,761.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe

Japan

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ametoa tamko rasmi la utatanishi juu ya michezo ya Tokyo Olympics, ambalo waandaaji wameahirisha kwa mwaka mmoja baada ya kugundua hakuna njia salama ya michezo hiyo kufanyika kuanzia Julai.

“Michezo ya Olympic lazima ifanyike katika namna ambayo itaonyesha kuwa ulimwengu umeshinda vita vyake dhidi ya janga la virusi vya corona,” Abe ameliambia bunge.

Kauli yake imekuja siku moja baada ya mkuu wa Jumuia ya Madaktari ya Japan iliposema itakuwa vigumu kwa Japan kuwa mwenyeji wa Olympic mpaka pale itapopatikana chanjo na kutolewa kwa umma.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG