Kulingana na Shirika la Afya Duniani, WHO, karibu nusu ya watu waliofariki katika nchi za Ulaya ni watu wanaoishi katika nyumba za kulea watu wazima.
Akizungumza na waandishi habari hii Ijumaa kutokea mjini Copenhagan mwakilishi wa WHO katika nchi za Ulaya Hans Kluge amesema huko Ulaya, Itali, imeshuhudia idadi ya waliopona kwa siku imezidi idadi ya waliofariki kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa janga hilo nchini humo.
Uturuki imeshuhudia kuongezeka kwa wagonjwa kufikia watu laki moja siku ya Alhamisi na kuwa nchi ya saba duniani yenye wagonjwa wengi ikiipita Iran huko mashariki ya kati.
Wakati huohuo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amepongeza uamuzi wa viongozi wenzake wa Umoja wa Ulaya kwa kufikia maridhiano juu ya mpango wa kuokoa uchumi wa nchi zao kutokana na athari za janga la virusi vya Coorna.
Viongozi wa EU wamaitaka kamisheni ya umoja huo kutayarisha mpango wa dharura wa pamoja kukabiliana na athari za janga la virusi vya corona na kuunganisha mfuko wa dharura kupambana na janga hilo katika bajeti ya muda mrefu ya 2021.
Viongozi hao walikubaliana jana kimsingi wakati wa mkutano kupitia teknolojia ya mawasliano kwa video juu ya bajeti hiyo kwa kuidhinisha mpango wa dola bilioni 587 uliotayarishwa na mawaziri wa fedha wa EU ili kunusuru makampuni ya ulaya na wafanyakazi wake.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC