Wanaharakati na wanasayansi wa mazingira wanasema uchafuzi wa mazingira umepungua kwa kiwango kikubwa pale watu wengi walipolazimika kubaki nyumbani.
Katika kuadhimisha siku hii mashirika ya kutetea mazingira yanatoa wito kwa mataifa ya dunia kuweka azma ya kutumia nishati mbadala.
Siku ya Dunia huadhimishwa Aprili 22 kila mwaka kwa shughuli mbalimbali za kuimarisha mazingira duniani kote.
Wanaharakati hao wanaeleza kwamba ukosefu wa magari njiani na kufungwa viwanda ni ushahidi kwamba kunahitajika mabadiliko makubwa katika tabia ya binadamu kutokana na jinsi hewa imebadilika katika miji mikubwa duniani.
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, linaeleza katika taarifa yake kwamba janga hili la virusi vya corona linakumbusha binadamu jinsi alivyo mdhaifu na hatari zinazoikabilli dunia.
Kutokana na janga hilo mwaka hug hakuna sherehe za kawaida za kuhamasisha usafi wa mazingira kama zinavyofanyika katika miaka ya nyuma.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.