Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:53

Utabiri wa hali ya hewa waonyesha dhoruba zaidi kutokea Marekani


Athari zilizoachwa na dharuba iliyoambatana na upepo mkali huko Oklahoma, Marekani Mei 26, 2019.
Athari zilizoachwa na dharuba iliyoambatana na upepo mkali huko Oklahoma, Marekani Mei 26, 2019.

Watabiri wa hali ya hewa Marekani wanaonya juu ya uwezekano wa kutokea dhoruba hatari zaidi kwenye maeneo ya katikati ya nchi, inayoambatana na upepo mkali katika maeneo ambayo yalishuhudia hali ya hewa mbaya sana Jumatatu usiku.

Idara ya hali ya hewa Marekani-NWS imeeleza Jumanne vimbunga takribani 53 ambavyo huenda vimepiga usiku kucha, vimeuwa mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 90.

Ripoti za dhoruba zilibandikwa kwenye mtandao na kitengo cha utabiri wa majanga cha taifa, zimeeleza kwamba vimbunga vilivyotabiriwa 14 vilipiga kwenye jimbo la Indiana, 11 Colorado na tisa Ohio.

Vimbunga 6 viliripotiwa kwenye jimbo la Iowa, vitano Nebraska, vinne huko Illinois, vitatu Minnesota na kimoja kwenye jimbo la Idaho.

Dhoruba hiyo iliharibu nyumba, kung’oa miti na kuangusha nguzo za umeme na kupelekea vifusi vingi ambavyo timu ya wasafishaji iliwabidi kutumia vifaa vya kuzolea theluji kusafisha barabara kuu huko Ohio.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG