Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:24

Kimbunga Michael : Idadi ya vifo yafikia 11 Florida


Waokoaji wakiwa katika eneo ambalo limeharibiwa na Kimbunga Michael, katika pwani ya Mexico, Florida, Octoba 11, 2018.
Waokoaji wakiwa katika eneo ambalo limeharibiwa na Kimbunga Michael, katika pwani ya Mexico, Florida, Octoba 11, 2018.

Wakazi na wafanyakazi wa idara ya uokoaji huko Florida na maeneo mengine ya kusini mashariki ya majimbo ya Marekani yako katikati ya harakati za kurekebisha maeneo ambayo yameharibiwa na kimbunga Michael.

Sehemu ya kimbunga Michael baada ya kutua Florida kilielekea katika Bahari ya Atlantic.

Michael ili sababisha vifo vya watu 11 baada ya kimbunga hicho kuwasili kwa kishindo Jumatano kikiwa katika daraja la 4 jimboni Florida na kuvuka kuelekea maeneo ya Georgia, Carolina na Virginia ikiwa bado kina kasi ya juu.

Wafanyakazi wa huduma za dharura waliendelea kuchimba na kufukuwa katika eneo lote ambalo nyumba na majengo yalikuwa yameanguka wakiwatafuta watu ambao wamenusurika.

“Nina tarajia idadi ya walio kufa itaongezeka siku ya leo,” Kiongozi wa Idara ya serikali kuu inayo simamia huduma za dharura Brock Long amesema Ijumaa kupitia televisheni ya CNN.”

“Tunaomba kuwa idadi hiyo isiongezeke zaidi, lakini uko uwezekano huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa nyumba zimeharibiwa kabisa katika mji wa Mexico Beach, mahali kimbunga kilitangulia kutua, barabara zikiwa zimezibwa na miti, na milingoti ya umeme iliyokuwa imeanguka.

XS
SM
MD
LG