Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:29

Maporomoko yauwa watu zaidi ya 40 Uganda


Ramani inayo onyesha Wilaya ya Bududa, palipo tokea maporomoko ya matope.
Ramani inayo onyesha Wilaya ya Bududa, palipo tokea maporomoko ya matope.

Maporomoko ya matope yaliotokea upande wa mashariki mwa Uganda yameuwa watu zaidi ya 40 kufikia siku ya Ijumaa.

Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi, saa nane mchana katika wilaya ya Bududa, kijiji cha Bukalasi, katika mlima Elgon. Wakazi wa eneo hilo wamesema maporomoko hayo yaliambatana na mvua kubwa.

Walio shuhudia wamesema kwamba maji, udongo pamoja na miti, viliporomoka kutoka juu ya m lima hadi chini mtoni, na kusababisha maafa makubwa ikiwemo mimea na mifugo kuzikwa wakiwa hai.

Hata hivyo vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa mvua kubwa zinazo endelea kunyesha katika eneo hilo zimezuia zoezi zima la kuwaokoa wale walioathirika na janga hilo.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya ya Bududa, kata ndogo ya Bukalasi, yenye milima mingi, maporomoko ya matope yalianza kushuhudiwa saa nane alasiri Alhamisi, wakati maji, matope, na miti ikiporomoka kutoka juu ya mlima, kufunika makao ya watu hadi sehemu tambarare madukani.

Hadi tukiandaa taarifa hii, maafisa wa uokoaji walikuwa hawajafika eneo la tukio, wakazi wa eneo hilo wenye ujasiri wakijitwika jukumu la kuwaokoa wenzao.

“Nyumba zimefunikwa na udongo. Kituo cha kibishara nacho kimefunikwa kiasi kwamba huwezi kujua kama kilikuwepo. Kwa sasa tunaogopa kuwaokoa wenzetu kwa sababu huwezi kujua, maporomoko makubwa Zaidi yanaweza kutokea tena,” ameongezewa Wakikona.

XS
SM
MD
LG