Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:17

Watatu wapoteza maisha katika tetemeko lingine Indonesia


Tetemeko Indonesia
Tetemeko Indonesia

Watu watatu wamepoteza maisha baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea nje kidogo ya visiwa vya Java na Bali nchini Indonesia, hali iliyo ongeza majonzi kwa wakazi wa kisiwa hicho ambacho kimeemewa kutokana na maafa.

Majanga yote matatu yametokea huko Java, ambako nyumba kadhaa zilizoko wilaya ya Sumenep ziliharibiwa na tetemeko la asubuhi na mapema lenye ukubwa wa 6.0.

Maelfu ya wanaotembelea kisiwa cha Bali, ambacho huwa ni mwenyeji wa mikutano ya kila mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) walikimbia kuelekea nje ya hoteli zao kwa hofu ya kuwa majengo yalikuwa yakitikisika na kutetemeka.

Hapana taarifa ya mara moja ilioeleza uharibifu katika eneo hilo la Bali, na hakuna tahadhari yoyote ya tsunami iliyo tolewa.

Janga la Alhamisi lilitokea wakati waokoaji walikuwa wakimaliza siku yao ya mwisho wakitafuta miili iliyo kuwa imebakia katika kisiwa cha Sulawesi, ambapo zaidi ya watu 2,000 waliuwawa katika tetemeko na wimbi kubwa la tsunami la mwezi uliopita lililoleta uharibu mkubwa.

Uharibifu huo kwa sehemu kubwa ulitokea katika mji wa Palu, ambako nyumba kadhaa zilifunikwa wakati tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.5 lilipotokea na kubadilisha eneo lenye unyevunyevu kuwa ni mto wenye matope.

Maafisa wanaamini kuwa watu wapatao 5,000 inawezekana kuwa walizikwa katika udongo huo laini.

Zoezi la kuwatafuta wahanga ilikuwa limalizike Alhamisi, lakini msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa amesema limeongezwa muda hadi Ijumaa kwa maombi yaliyoletwa na familia hizo ambazo bado wanaendelea kuwatafuta ndugu zoa wapenzi.

Takriban wakazi 500 waliuwawa na mtiririko wa matetemeko yaliyo ikumba kisiwa cha Lombok kati ya Agosti na Septemba.

XS
SM
MD
LG