Watu hao wamethibitishwa kupoteza maisha na vyombo vya dola vikihofia idadi hiyo kuongezeka kadiri waokoaji wakifanya bidii kuzifikia jamii zilizo maeneo ya mbali, yasiyo kuwa na mawasiliano wala misaada.
Dazeni ya watu wameripotiwa kuwa wamekwama katika kifusi cha majengo mawili ya hoteli na maduka ya biashara katika mji wa Palu, ambao ulipitiwa na mawimbi yenye urefu wa mita sita (futi 20) baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 7.2 kutokea Ijumaa.
Rais wa Indonesia Joko “Jokowi” Widodo ametembelea Palu Jumapili.
“Kuna changamoto nyingi,” Jokowi amesema. “Inabidi tufanye vitu vingi mapema, lakini hali iliyopo haituruhusu kufanya hayo.”
Mwanamke mwenye umri mdogo alitolewa akiwa hai kutoka katika kifusi cha hoteli iliyo bomoka ya Roa Roa, tovuti ya habari Detik.com imeripoti.
Mmiliki wa hoteli Ko Jefry ameiambia Televisheni ya Jiji Jumamosi kuwa watu sitini wanasadikiwa kuwa wamekwama katika kifusi hicho. Mamia ya watu walikusanyika katika uwanja wenye maduka ya biashara wakiwatafuta watu wawapendao.