Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:16

Watu 384 wapoteza maisha kufuatia tetemeko, tsunami Indonesia


Msemaju wa kitengo cha maafa Indonesia, Sutopo Purwo Nugroho akieleza hali ilivyo baada ya tetemeko katika mkutano na waandishi wa habari, Septemba 29, 2018.
Msemaju wa kitengo cha maafa Indonesia, Sutopo Purwo Nugroho akieleza hali ilivyo baada ya tetemeko katika mkutano na waandishi wa habari, Septemba 29, 2018.

Maafisa wa Indonesia wamesema kuwa watu wasio pungua 384 wamepoteza maisha na wengine 540 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 7.5 liliotokea Ijumaa na kufuatiwa na kishindo cha wimbi kubwa la tsunami katika miji miwili – Palu na Donggala – eneo la kati la jimbo la Sulawesi.

Vyombo vya usalama vimesema Jumamosi mamia ya watu walikuwa kwenye ufukwe wa Palu wakiwa katika tafrija wakati tetemeko hilo lilipozuka na wimbi kubwa la tsunami kulikumba eneo hilo, likiwazoa watu wengi na kupoteza maisha.

Msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa Sutopo Purwo Nugroho amesema kuwa tsunami hiyo ilikuwa ina safari kilomita 800 kwa saa, na limeharibu majengo na miundo mbinu.

Amesema maelfu ya nyumba, hospitali na sehemu za maduka makubwa na hoteli ziliharibiwa kabisa na kuanguka na maporomoko hayo yamekata njia kuu inayo unganisha Palu.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa jitihada za uokoaji bado zinaendelea ingawa bado zipo changamoto za kukatika kwa umeme na kukosekana kwa mawasiliano kutokana na daraja kuu linalo unganisha eneo hilo la tukio kuharibiwa na kuanguka.

XS
SM
MD
LG