Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:48

Tetemeko : Zoezi la kuokoa wapanda mlima laendelea Indonesia


Wananchi wa Indonesia na wapanda milima kutoka nje ya nchi baada ya kushuka kutoka mlima wa Rinjani.
Wananchi wa Indonesia na wapanda milima kutoka nje ya nchi baada ya kushuka kutoka mlima wa Rinjani.

Shughuli za uokoaji zinaendelea kwenye kisiwa cha Lombok nchini Indonesia ambapo wapanda mlima na wanaoongoza misafara hiyo, wamekwama kwenye mlima wa Rinjani.

Misafara hiyo imekwama kutokana na tetemeko zito la ardhi lililotikisa eneo la mlima huo na kusababisha maporomoko ya ardhi na vifo vya watu 162.

Mkuu wa mbuga ya wanyama Rinjani amesema kwamba watu wasiopungua 500, wengi wakiwa raia kutoka nje ya Indonesia, wamekwama kwenye mlima huo wa Volcano ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Indonesia.

Ripoti zinasema kwamba zaidi ya nyumba 1000 zimeharibiwa vibaya.

Tetemeko la ardhi lenye urefu wa kilomita saba kwenda chini ya ardhi, limetikisa kisiwa cha Lombok, chenye shughuli nyingi za kitalii siku ya jumapili, na kusababisha watu kukimbilia maeneo yaliyo salama.

Maafisa wanasema kwamba sehemu hiyo imekubwa na mtikisiko mara 124 baada ya tetemeko hilo la ardhi.

XS
SM
MD
LG