Kimbunga hicho cha kihistoria, ambacho kinatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa kimeathiri shughuli zote katika mji wa Houston huku waokozi wakijaribu kuwafikia manusura waliokwama kwenye mafuriko hayo.
Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia kwamba kimbunga Harvey, ambacho kiliikumba Texas Ijumaa usiku huenda kikasababisha hadi centimita 25 za mvua.
Kimpunga hicho kimesababisha mafuriko zaidi kwenye mji huo ulio wa nne kwa ukubwa nchini Marekani.
Kwa mujibu wa kituo cha hali ya hewa baadhi ya maeneo tayari yameshuhudia zaidi ya centimita 60 za mvua.
Afisa mkuu wa kituo cha utabiri wa hali ya hewa cha Marekani, Patrick Burke, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba kati ya centimita 40 na 60 za mvua zinatarajiwa kushuhudiwa kufikia Jumatano wiki hii.