Katika mji mkuu wa Uingereza - London, kiwango cha joto kimefikia nyuzi joto 37.7, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa kote Uingereza mwezi Julai.
Hii ni rekodi ya pili ya juu ya joto tangu Agosti 10, 2003, wakati kiwango cha joto kilifikia nyuzi joto 38.5 katika mji wa Faversham.
Katika hali ya kukabiliana na joto hilo watu wanakula barafu ili kupunguza joto mwilini na pia kwenda katika maeneo yenye upepo kama vile kando ya mito na bahari.
Kulingana na utabiri wa hali ya hewa, Kiwango cha juu cha joto ulaya, kinatarajiwa kuendelea kwa mda wa miezi mitatu hadi Oktoba.
Kituo cha utabiri wa hali ya hewa nchini Ufaransa kilisema Alhamisi hali ya joto itaongezeka zaidi na kuweka rikodi mpya baadae wiki hii.
Watalii wamekuwa wakimiminika kwenye chemchem ya Trocadero chini ya mnara wa edible Eiffel kujikinga na joto.
Hata hivyo kwa mujibu wa utabiri huo joto linatarajiwa kumalizika mapema Ijumaa.