Watu wasiopungua 30 hawajapatikana baada ya tetemeko la 6.8 katika kipimo cha Rikta kutokea Ijumaa usiku, ambako chimbuko lake lilikuwa ni katika mji mdogo wa Sivrice ulioko pembeni ya ziwa mashariki ya jimbo la Elazig.
Mawaziri wa Mambo ya Ndani, Mazingira na Afya wa Uturuki, waliokuwa katika eneo la tukio la tetemeko, wamesema vifo vilitokea katika jimbo la Elazig na jimbo jirani la Malatya lilioko kusini magharibi..
Watu wasiopungua 20 walikufa na wengine 1,015 walijeruhiwa, kwa mujibu wa AFAD.
“Hakuna mwili uliochini ya kifusi katika mji wa Malatya, lakini juhudi za kutafuta miili na uokoaji zinaendelea katika mji wa Elazig kutafuta wananchi 30,” Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu alieleza Ijumaa.
Ilikuwa inatisha kwani samani zilizoko ndani ya jengo zilituangukia. Tulifanya haraka kutoka nje,” Melahat Can, 47, anayeishi jimbo la Elazig, ameliambia shirika la habari la AFP.
Rais Recep Tayyip Erdogan amesema hatua zote zimechukuliwa kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo, ambalo lilisababisha hofu maeneo yote.
Idara ya maafa na masuala ya dharura ya serikali ya Uturuki (AFAD) imesema tetemeko hilo lilipiga Sivrice mida ya saa 8:55 usiku (1755GMT). Uturuki iko katika ukanda ambao unapata matetemeko mara kwa mara.
Televisheni za Uturuki zilionyesha picha za watu wakikimbia nje ya majumba kutokana na hofu na pia moto uliokuwa unawake juu ya jengo.
Timu za waokoaji ziliendelea kuwatafuta waliokuwa wamekwama katika kifusi cha nyumba ya ghorofa tano katika Kijiji kilichoko kilomita 30 kutoka mji wa Elazig, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa shirika la AFP. Mtu mmoja alitolewa kaiwa hai kutoka katika kifusi.