Idara ya hali ya hewa na jiolojia, BMKG, imeripoti kuwa Tsunami imetokea karibu saa tatu na nusu usiku, nusu saa baada ya kulipuka kwa mlima wa volcano wa Anak Krakatoa.
Idara inaeleza kwamba huwenda tsunami imesababishwa na mchanganiko wa mambo ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa ardhi chini ya bahari baada ya mlipuko wa volcano pamoja na mawimbi makubwa yaliyo sababishwa na mwezi mpevu.
Msemaji wa idara ya kukabiliana na majanga ya kitaifa, BNBP, ameeleza kwamba mamia ya nyumba, hoteli 9 na zaidi ya boti 350 zimeharibika pamoja na mamia ya magari na vyombo vingine vya usafiri.
Rais Joko Widodo wa Indonesia ameamrisha idara zote za serikali kusaidia kwa haraka maeneo yaliyokumbwa na maafa.
Tsunami hiyo imetokea karibu na mahala ambako tetemeko kubwa la Disemba 26, 2004 pamoja na tsunami iliyofuata ilisababisha vifo vya watu 226, 000 katika nchi 13 pamoja na Zaidi ya 120,000 huko Indonesia.