Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:37

Watu zaidi ya milioni 6 wakabiliwa na njaa Sudan Kusini - Ripoti


Shirika la Chakula Duniani likisambaza msaada wa chakula kwa ndege katika maeneo yanayokabiliwa na janga la njaa katika mji wa Jiech, kaunti ya Ayod, Sudan Kusini.
Shirika la Chakula Duniani likisambaza msaada wa chakula kwa ndege katika maeneo yanayokabiliwa na janga la njaa katika mji wa Jiech, kaunti ya Ayod, Sudan Kusini.

Miaka minane baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake, njaa inaendelea kuiathiri nchi hiyo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha takriban nusu ya wakazi wa nchi hiyo – watu milioni 6.1- wanakabiliwa na kiwango fulani cha ukosefu wa chakula.

Tatizo la hali ya hewa, uchumi usiozorota, na vita katika baadhi ya sehemu Sudan Kusini zimepelekea mamilioni ya wakimbizi kuvuka nchi za jirani. Wengine wanatafuta chakula na usalama wao katika maeneo ya kuwalinda raia au POCs, ndani ya nchi.

Idadi iliyotolewa yaonyesha watu nchini Sudan Kusini wanakabiliwa na hali tete ya ukosefu wa chakula kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya serikali ya Sudan na Umoja wa Mataifa iliyotolewa Ijumaa.

Ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya watu milioni 7 au zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu wa nchi hiyo wako hatarini.

Thomson Phiri ni meneja mawasiliano wa shirika la chakula duniani, WFP, Sudan Kusini anasema : “

“Sudan Kusini ni moja ya program zenye matatizo ulimwenguni kwa WFP, kwa sababu asilimia 60 ya eneo la nchi hiyo haliwezi kufikiwa kwa njia ya barabara, wakati wote wa masika, na lakustaajabisha ni kuwa msimu wa mvua umesadifu kipindi cha njaa Sudan Kusini, wakati watu wakihangaika kutafuta mlo wao wa kila siku.”

Watu wenye njaa inahitaji hali ya dharura katika vituo vya kugawa chakula – Umoja wa Mataifa POC katika mji wa Malakal, Sudan Kusini – wakati wafanyakazi wa WFP wakitoa mgao wa chakula wa kila mwezi kwa watu waliokimbia makazi yao wanaoishi hivi sasa katika eneo hili.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC.

XS
SM
MD
LG