Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:35

Mkuu wa UN azitaka serikali kuchunga haki za binadamu wanapokabiliana na janga la corona


Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa na Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus (kulia) makao makuu ya WHO, Geneva, Uswiz, Februari 24, 2020. (Salvatore
Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa na Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus (kulia) makao makuu ya WHO, Geneva, Uswiz, Februari 24, 2020. (Salvatore

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mlipuko wa virusi vya corona “umeanza kwa kasi kuwa mgogoro wa haki za binadamu.”

Tamko la UN

Katika tamko lake Alhamisi, amezitaka serikali kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kufikiwa na watu wote, misaada ya kiuchumi inawasaidia wale walioathirika zaidi na janga hili na kila mtu anauwezo wa kupata chakula, maji na makazi.

“Tumeona jinsi virusi hivyo havibaguwi, lakini athari zake zinabagua – ikidhihirisha udhaifu mkubwa katika utoaji huduma za umma na kukosekana usawa katika miundo ya huduma hizo ambazo zinawazuilia wao kuzifikia. Ni lazima tuhakikishe masuala haya yanapatiwa ufumbuzi katika kukabiliana nayo,” Guterres amesema.

Ameongeza kuwa : “Yote yale tunayofanya, tusisahau : Tishio ni virusi na siyo watu.”

UN

Ujumbe kutoka kwa Mkuu wa UN umekuja wakati maafisa wa afya wameonya kuwa pamoja na kuwa baadhi ya nchi zimepiga hatua kubwa na zimeanza kulegeza masharti ya kutotoka nje, vita dhidi ya virusi hivi bado kabisa haijamalizika.

“Tusifanye makosa kabisa : tunasafari ndefu mbele yetu. Virusi hivi vitakuwa katika jamii yetu kwa kipindi kirefu,” amesema mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus.

“Nchi nyingi bado ziko katika hatua za mwanzo za mlipuko wao huu. Na baadhi waliokuwa tayari wameathirika katika janga hili hivi sasa wameanza kuona mlipuko mpya wa maambukizi.

Marekani

Maafisa wa afya Marekani wanawataka wananchi kujitayarisha na msimu wa mafua makali na kuchanja ili kusaidia kupunguza uwezekano wa rasilmali za afya kuelemewa iwapo kutakuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa mafua makali na virusi vya corona wakati mmoja.

Ilivyokuwa dalili za maradhi hayo zinafanana, Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi Robert Redfield amewaambia waandishi, “Itatulazimu tupambanue kati ya mafua makali na maambukizi ya virusi vya corona.”

“Ninataka watusaidie hivi sasa kutuandaa vyakutosha kuanza kupata chanjo ya mafua makali na kuiondoa sura ya mafua makali, amesema.

Nchi nyingi zimejikita katika kuzuia maambukizi ya hivi sasa kwa kuamrisha watu kutotoka nje.

Amri hizo zinafanya hali kuwa ngumu kwa shughuli za kila siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani wa Waislam.

Indonesia

Indonesia, nchi yenye Waislam wengi wengi zaidi duniani, imekataza mamilioni ya watu wanaoishi katika miji mikubwa kusafiri kurudi majumbani kwao. Maafisa katika mji mkuu wa Jakarta wameogeza muda wa kutotoka nje mpaka Mei 22 na kuwataka Waislam kuacha kwenda msikitini.

Uturuki

Waziri wa Afya wa Uturuki ametoa amri sawa na hizo za Indonesia, akisema watu waache utamaduni wa kufuturu na marafiki zao na familia zao katika mfungo wa Ramadhani hadi mwakani.

Uturuki imeweka amri ya kutotoka nje na kupiga marufuku vijana wenye umri chini ya miaka 20 na wazee walio na umri wa zaidi ya miaka 65 kutotoka majumbani.

Malaysia

Waislam katika mji mkuu wa Malaysia wametakiwa kusali majumbani na misikiti yao kuendelea kufungwa.

Pakistan

Pakistan imechukuwa hatua tofauti, ikipuuzia ombi la madaktari na kuendelea kuruhusu misikiti iwe wazi, lakini imekuwa ikiwahimiza watu kutokaribiana.

Suala la iwapo watu waruhusiwe kukusanyika kwa ajili ya ibada nchi nyingi zinakabiliana nalo, na miongoni mwa dini nyingi.

Makanisa Marekani

Maafisa nchini Marekani maeneo mengi imewataka watu kujiepusha na mikusanyiko wakati wa sikuku ya Kikristo ya Pasaka mapema mwezi huu, wakati baadhi ya makanisa yamekaidi amri ya kutotoka nje na kuendesha ibada hizo makanisani.

California

Jaji wa Mahakama Kuu California amesema Jumatano atatupilia mbali ombi la makanisa matatu linalotaka amri ya mahakama kusitisha kwa muda amri ya gavana. Wanadai kuwa serikali inavunja Haki ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba ya uhuru wa kuabudu na kukusanyika.

Lakini Jaji amesema wakati huu wa hali ya dharura, serikali inayo mamlaka ya “kutoa suluhisho la dharura, ambalo linaweza kukandamiza haki za msingi za kikatiba.”

XS
SM
MD
LG