Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:53

Spain yalenga kulegeza masharti ya kutotoka nje kudhibiti COVID-19 mwezi Mei


Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez akihutubia bunge la nchini hilo mjini Madrid on April 22, 2020.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez akihutubia bunge la nchini hilo mjini Madrid on April 22, 2020.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez analenga ifikapo kipindi cha pili cha mwezi Mei “kufikia upeo wa kupunguza maambukizi,” wakati serikali yake na wengine wakianza kupanga kulegeza masharti magumu yaliyowekwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Akizungumza katika bunge Jumatano wakati akiomba muda wa amri ya kutotoka nje uliowekwa hivi sasa uongezwe hadi Mei 9, Sanchez amesema Uhispania ikianza kulegeza masharti mchakato utakuwa “hatua kwa hatua.”

Hilo litakwenda sambamba na tahadhari zilizotolewa na maafisa wa afya wa umma ambao siku za karibuni wamezitaka serikali kuwa waangalifu katika kulegeza masharti upande wa biashara na shughuli za umma, wakisema kuwa kuharakisha hilo kunahatarisha kuzuka maambukizi mapya.

Uhispania imekuwa moja kati ya nchi zilizoathirika vibaya zaidi na maambukizi duniani, ambapo kuna maambukizi 208,000 yaliyothibitishwa ya COVID-19 na vifo visivyo pungua 21,700.

Masharti ya kutotoka nje yalitangazwa katikati ya mwezi Machi.

Baadhi ya biashara zimeruhusiwa kufunguliwa, na baada ya ukosoaji kutoka kwa wananchi serikali imesema kuanzia Jumapili watoto chini ya miaka 14 wataruhusiwa kutoka nje kutembea.

Wakati ambapo nchi nyingi duniani zimejikita katika programu za kupima kutambua maambukizi, kuwatenga walioambukizwa na kufuatilia wale waliokuwa wamekaribiana nao, kuna wasiwasi juu ya maeneo ambapo upimaji wa umma haupo na watu wanaishi kwa kuchanganyikana.

Hii ni pamoja na makambi ya wakimbizi, na Jumatano shirika la Umoja wa Mataifa (UN) linalowasimamia wakimbizi wa Palestina limeripoti ambukizi lililothibitishwa la mtu wa kwanza katika kambi mmoja mashariki ya Lebanon.

Shirika hilo limesema mwanamke ni Mpalestina kutoka Syria na amepelekwa hospitali mjini Beirut. Limeongeza kuwa linachukuwa hatua muhimu zinazohitajika kuwasaidia familia yake kujitenga na misongamano, na kwamba inapeleka timu ya wataalam kuchukuwa vipimo vya virusi vya corona.

Serikali pia zinania ya kutafuta chanjo ya COVID-19, hatua muhimu itakayo epusha milipuko mikubwa siku za usoni.

Robert Redfield, mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Maradhi (CDC), ameliambia gazeti la Washington Post Jumanne kuwa wimbi la maambukizi baadae mwaka huu wakati kipindi cha flu kikianza “kinaweza kuwa kigumu zaidi” na kufanya mfumo wa afya kuelemewa zaidi.

Marekani na China ni kati ya nchi ambazo hivi sasa zinafanya majaribio ya chanjo za virusi vya corona, wakati maafisa wakisema huenda tafiti hizi zikaendelea angalau hadi mapema mwaka ujao kabla ya chanjo hiyo kuwa tayari kutolewa kwa umma.

Maafisa wa afya Uingereza wamesema Chuo Kikuu cha Oxford kimepanga kuanza majaribio ya aina moja ya chanjo itakayotolewa kwa watu Alhamisi.

“Katika hali ya kawaida, kufikia hatua hii ingechukua mwaka mzima,” Waziri wa Afya Matt Hancock amewaambia waandishi.

Amekumbusha kuwa kutengeneza chanjo ni mchakato unafanywa “kwa majaribio na kisha kurejea majaribio hayo tena.”

XS
SM
MD
LG