Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:00

Maelfu ya wafungwa waachiliwa huru Cameroon kwa hofu ya maambukizi ya Corona


Rais wa Cameroon Paul Biya
Rais wa Cameroon Paul Biya

Maelfu ya wafungwa wa Cameroon wameachiwa huru kama ilivyoamriwa na Rais wa nchi hiyo  Paul Biya, baada ya serikali yake kuripoti kwamba janga la virusi vya corona lilikuwa linaenea kwa kasi na wafungwa walikuwa miongoni mwa vikundi vilivyoambukizwa  kwa kiwango cha juu.

Serikali haijatoa idadi ya wafungwa walioambukizwa lakini inasema zaidi ya watu 1,500 wamekutwa na virusi vya COVID-19 nchini humo chini ya miezi miwili, na vifo zaidi ya 50.

Gereza kuu la Bamenda lina wafungwa 403 waliotangazwa rasmi. Cameroon ina magereza 78 yaliyokuwa yamejaa sana na wafungwa 30,000 katika vituo vya mahabusu ambavyo vilijengwa ili kuwahifadhi wafungwa wapatao 9,000 tu.

Kati ya watu 1,400 waliopata uhuru wao kutoka kwenye magereza ya Bamenda, Bafoussam, Bertoua na Buea ni Emmanuel Ngomba anayesema alikamatwa miaka miwili iliyopita, akiwa na miaka 16, na kushikiliwa katika Gereza Kuu la Buea.

“Nilitoka nyumbani jioni moja kwenda kuonana na rafiki. Alisema kwamba tunataka kwenda kuchukua vitu kutoka kwa duka la mjomba wake. Tulikwenda huko, tukachukua chupa za gesi na mafuta ya injini. Polisi walinikamata. Gereza sio mahali pazuri,” alisema.

Ngumba, ambaye alizungumza kupitia App moja ya kutuma ujumbe, alisema alinyimwa haki zake kwa sababu anatuhumiwa kwa wizi na alifungwa gerezani kwa miaka miwili bila kufungulia mashtaka.

Pierre Tchamba mwenye umri wa miaka hamsini na mbili pia alipata uhuru baada ya zaidi ya miaka 24 katika gereza la Bertoua, ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kuua bila kukusudia na wizi wa kutumia nguvu.

Tchamba anasema baada ya miaka 24 na miezi minne ya kuwekwa kizuizini katika hali ya kinyama, hatimaye amepata uhuru wake wa shukran kwa COVID-19, ambayo imekuwa ikienea nchini Cameroon na kuwaambukiza wafungwa.

Mkutano wa dharura uliosimamiwa na Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute wiki iliyopita ulitangaza kwamba COVID-19 ilikuwa tishio katika magereza ya Cameroon lakini haukusema ni wafungwa wangapi walikuwa wameambukizwa au kufa kutokana na janga hilo.

Mnamo Aprili 15, Rais Biya aliamuru kuachiliwa kwa maelfu ya wafungwa kutokana na wasiwasi juu ya msongamano unavyoeneza korona.

Chini ya uamuzi wa rais, vifungo vya maisha vilipunguzwa kwa miaka 25 na wale ambao vifungo vya maisha vilipunguzwa hadi miaka 25 waliondolewa miaka mitano kwenye hukumu zao.

Hukumu za miaka kumi zilipunguzwa kwa miaka mitatu, vifungo vya miaka mitano vikapunguzwa kwa miaka miwili na hukumu za miaka mitatu zilikatwa kwa mwaka mmoja.

XS
SM
MD
LG