Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:54

Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris barani Afrika

Ziara yake nchini Ghana na leo Tanzania na baadaye nchini Zambia inafuatia mkutano wa mwezi Disemba ulioandaliwa na Rais Joe Biden mjini Washington pamoja na viongozi wa Afrika ili kupunguza ushawishi wa China na Russia unaoongezeka barani Afrika.

Makamu wa Rais wa Marekani alifanya safari ya kuongozwa kwenye Kasri ya Cape Coast, eneo lililotajwa na shirika la Sayansi, elimu na utamaduni la Umoja wa mataifa (UNESCO) kuwa urithi wa dunia ambako watumwa walikuwa wanasafirishwa kuelekea kaskazini na kusini mwa Amerika na eneo la Caribbean.

Aliweka shada la maua kuwaenzi wale waliofariki wakati wa biashara ya watumwa.

“Ukatili wa kile kilichotokea hapa lazima ukumbukwe,” Harris alisema kwa maneno mazito, akizungumza kwa sauti ya uchungu na karibu atokwe na machozi.


Makundi

XS
SM
MD
LG