Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:37

Rais Biden awasili Ireland kuunga mkono na kusherehekea mkataba wa amani


Rais Joe Biden alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Belfast, Ireland ya Kaskazini, April 11, 2023.
Rais Joe Biden alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Belfast, Ireland ya Kaskazini, April 11, 2023.

Rais wa Marekani Joe Biden anasafiri kwenda pande zote mbili za mpaka wa Ireland wiki hii, akishiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 25 ya mkataba wa amani Good Friday wa Ireland ya Kaskazini, akifanya hija katika miji ya wahenga wake huko Ireland.

Ziara ya Biden inakuja wakati uhimilivu wa mkataba wa amani huo ukipitia majaribio kutokana na hitilafu za kisiasa na mashambulizi ya baadhi ya matukio yaliyofanywa na waasi.

Ghasia za hivi karibuni zimetokea Jumatatu wakati vijana waliokuwa wamefunika nyuso zao walizitupia mawe gari za polisi kwa kutumia mabomu ya petrol wakiwa wanaandamana huko Londonderry.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amepangiwa kumkaribisha Biden atakapo wasili Jumanne usiku mjini Belfast. Siku ya pili Biden atafanya mkutano wa pande mbili na Sunak kabla ya kuhutubia Chuo Kikuu cha Ulster mjini Belfast.

Makubaliano ya Good Friday – ambayo Marekani ilisaidia kufikiwa Aprili 10, 1998 – yalimaliza kwa kiasi kikubwa miongo kadhaa ya ghasia za madhehebu ambazo ziliigubika Ireland Kaskazini tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 na pia zilisababisha mashambulizi ya mara kwa mara kwa Uingereza bara. Wakati bado kuna ghasia za hapa na pale huko Ireland Kaskazini, mkataba huo ulikiwezesha kizazi cha watoto kukulia katika mazingira ya amani.

Licha ya mafanikio ya mkataba huo, umekuwa katika mvutano unaoongezeka tangu Uingereza ilipojitoa kutoka Umoja wa Ulaya na kutokubaliana juu ya kanuni za biashara katika kipindi hiki wakiwa nje ya Umoja wa Ulaya- Brexit.

Bunge la Ireland Kaskazini limekwama kwa zaidi yam waka baada ya chama kikuu cha unionist kilipojitoa serikalini kupinga kanuni mpya za biashara.

Baadhi ya taarifa hizi katika ripoti hii zimetokana na mashirika ya habari ya AP, Reuters na AFP.

XS
SM
MD
LG