Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:53

Ziara ya rais Biden, Ireland, kumkutanisha na binamu yake


BIDEN-INTELIGENCIA ARTIFICIAL
BIDEN-INTELIGENCIA ARTIFICIAL

Ziara ya rais wa Marekani, Joe Biden, iliyopangwa kufanyika wiki ijayo kwenda Ireland, inatarajiwa kumkutanisha na binamu yake wa mbali Joel Blewitt anayeishi katika mji wa Balina.

Rais Joe Biden atasimama Balina, mji ambao mababu zake walitokea huko na kuhamia Marekani katika miaka ya 1850.

Kwa sasa binamu wa rais Biden, Joel, anapokea simu nyingi kutoka kwa wakazi, na vyombo vya habari duniani kufahamu maamndalizi ya kumpokea ndugu yake ambaye ni rais wa 46 wa Marekani.

Ndugu hao waliwahi kukutana mwaka 2016, wakati huo rais Biden, akiwa makamu wa rais na kuahidi kwamba atarejea tena katika mji huo endapo atafanikiwa kuwa rais.

Joel Blewitt mwenye umri wa miaka 43, ana jishughulisha na ufundi bomba, alikuwa miongoni mwa waalikwa wa kiuhusiano katika White House wakati wa maadhimisho ya siku ya mtakatifu Patrick mwezi uliopita.

Binamu wa rais Joe Biden, Joe Blewitt,
Binamu wa rais Joe Biden, Joe Blewitt,

XS
SM
MD
LG