Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:03

Marekani itatumia dola milioni 690 kuimarisha demokrasia ulimwenguni-Biden


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano alifungua mkutano wake wa pili kuhusu demokrasia, akiahidi kwamba Marekani itatumia dola milioni 690 mwaka ujao kuimarisha harakati za demokrasia ulimwenguni.

Biden amesema “Tunabadili hali ilivyo hapa, kama tusemavyo kila mara, tuko katika hali isiyo ya kawaida katika historia, ambapo maamuzi tunayochukua leo yataongoza mwelekeo wa ulimwengu wetu kwa miongo kadhaa ijayo bila shaka.”

White House imebaini kuwa Marekani haswa inataka teknolojia isaidie kuimarisha demokrasia na sio kwa kupinga demokrasia.

Katika muktada huo, mawaziri wakuu wa nchi nane za Ulaya wamesaini barua na kuiwasilisa kwa wakuregenzi watendaji wa kampuni kubwa za mitandao ya kijamii wakiwataka kuchukua hatua madhubuti kwa kuzuia usambazaji wa habari za uongo kwenye mitandao yao.

Barua hiyo imesainiwa na viongozi wa Ukraine, Moldova, Poland, Jamhuri ya Czech, Estonia, Latvia, Lithuania na Slovakia.

Viongozi 120 wa dunia ndio walishiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao.

XS
SM
MD
LG