Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:09

Rais wa Marekani akutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Belfast


Rais wa Marekani Joe Biden atembelea Ireland ya Kaskazini.
Rais wa Marekani Joe Biden atembelea Ireland ya Kaskazini.

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na waziri mkuu wa uingereza Rishi Sunak mjini  Belfast, Ireland  Kaskazini  leo kama sehemu ya kuadhimisha miaka 25 ya makubaliano ya amani ya mwaka 1998 ya Ireland kaskazini.

Biden anayejivunia sana asili yake ya Ireland atatumia zaidi ya nusu siku katika eneo la Uingereza kabla ya kusafiri kwenda kusini katika jamhuri ya Irelanda kwa siku mbili na nusu za hotuba na mikutano na maafisa na kukutana na ndugu wa mbali.

Kusimama kwake kwa muda mfupi mjini Belfast kunakuja huku kukiwa na kukwama kwa kisiasa hivi karibuni ambao ulihusu kushirikiana madaraka, kiini cha mkataba wa amani wa mwaka 1998, hatua ambayo haijtekelezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na mzozo kuhusu mipango ya biashara baada ya brexit.

Kuondoka kwa uingereza katika Umoja wa ulaya kwa kiasi Fulani kuliharibu uhusiano kati ya uingereza na ikulu ya Marekani , wakati London na brussels zikihangaika kutafuta makubaliano ya kuachana ambayo hayataharibu kanuni za makubaliano ya amani.

Makubaliano ya Good Friday – ambayo Marekani ilisaidia kufikiwa Aprili 10, 1998 – yalimaliza kwa kiasi kikubwa miongo kadhaa ya ghasia za madhehebu ambazo ziliigubika Ireland Kaskazini tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 na pia zilisababisha mashambulizi ya mara kwa mara kwa Uingereza bara. Wakati bado kuna ghasia za hapa na pale huko Ireland Kaskazini, mkataba huo ulikiwezesha kizazi cha watoto kukulia katika mazingira ya amani.

Licha ya mafanikio ya mkataba huo, umekuwa katika mvutano unaoongezeka tangu Uingereza ilipojitoa kutoka Umoja wa Ulaya na kutokubaliana juu ya kanuni za biashara katika kipindi hiki wakiwa nje ya Umoja wa Ulaya- Brexit.

Bunge la Ireland Kaskazini limekwama kwa zaidi yam waka baada ya chama kikuu cha unionist kilipojitoa serikalini kupinga kanuni mpya za biashara.

XS
SM
MD
LG