Rais wa Kenya William Ruto, Alhamisi amemteua Douglas Kanja, kuwa Inspekta Jenerali wa polisi, ofisi yake imesema, ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mkuu wa zamani Japhet Koome, aliyejiuzulu kufuatia shutuma kwa namna alivyoshughulikia maandamano dhidi ya serikali.