Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:47

Ruto amteua Douglas Kanja kuwa Insepkta mpya wa polisi


Rais wa Kenya, William Ruto. AFP, Julai 11, 2024
Rais wa Kenya, William Ruto. AFP, Julai 11, 2024

Rais wa Kenya William Ruto, Alhamisi amemteua Douglas Kanja, kuwa Inspekta Jenerali wa polisi, ofisi yake imesema, ili  kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mkuu  wa zamani Japhet Koome, aliyejiuzulu kufuatia shutuma kwa namna alivyoshughulikia maandamano dhidi ya serikali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Kanja ambaye amekuwa akikaimu wadhifa huo tangu katikati ya mwezi Julai, ni polisi mwenye uzoefu wa karibu miongo minne, aliyewahi kuhudumu kama naibu mkuu wa polisi na pia kamanda wa kikosi cha GSU.

Makundi ya kutetea haki za binadamu ya Kenya hata hivyo yamedai kuwa vifo kutokana na maandamano hayo ni takriban 50. Maandamano nchini Kenya yameendelea kushuhudiwa hata baada ya Ruto, kuuondoa mswaada wenye utata wa fedha, pamoja na kufuta karibu baraza lake lote la mawaziri.

Wanaharakati wanadai kuwa wanataka Ruto ajiuzulu, huku wakidai mabadiliko ya kiutawala kushugulikia ufisadi pamoja na usimamizi wa serikali kuu, pamoja na zile la kaunti.

Forum

XS
SM
MD
LG