Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 07, 2024 Local time: 11:55

Ruto ameteua mawaziri kutoka chama kikuu cha upinzani ODM chake Raila Odinga


Rais wa Kenya William Ruto akizungumza katika ikulu ya rais ya Nairobi. July 11, 2024.
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza katika ikulu ya rais ya Nairobi. July 11, 2024.

Rais wa Kenya Dr. William Ruto, amemteua John Mbadi kuwa waziri wa fedha katika baraza la mawaziri ambalo linajumulisha wanasiasa kutoka muungano wa vyama vya upinzani.

Uteuzi mpya wa Ruto unalenga kujibu madai ya waandamanaji ambao wamekuwa wakiandamana katika nchi hiyo ya Afrika mashariki katika wiki za hivi karibuni.

Ruto amesema uteuzi wake unajumulisha kila mtu, baada ya kuvunja baraza lake la mawaziri mapema mwezi huu kutokana na matakwa ya waandamanaji vijana.

Maandamano hayo ndio mtihani mkubwa kwa utawala wa Ruto ambaye amekuwa madarakani kwa muda wa miaka miwili sasa.

Ruto vile vile amesema kwamba atapendekeza mabadiliko kwa sheria za kupambana na ufisadi za Kenya.

Wengine walioteuliwa kutoka chama cha upinzani cha ODM ni aliyekuwa gavana Wycliffe Oparanya kama waziri wa vyama vya ushirika, Opiyo Wandayi kama waziri wa nshati na mafuta, na Haasan Joho kuwa waziri wa madini na uchumi unaotokana na rasilmali za baharini.

Chama cha ODM kinaongozwa na Raila Odinga.

Forum

XS
SM
MD
LG