Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 03:50

Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram aendelea kushikiliwa nchini Ufaransa


Mwanzilishi wa mtandao wa kutuma ujumbe wa Telegram, Pavel Durov.
Mwanzilishi wa mtandao wa kutuma ujumbe wa Telegram, Pavel Durov.

Waendesha mashtaka wa Ufaransa Jumatatu walisema Pavel Durov, mwanzilishi wa mtandao wa Telegram na mzaliwa wa Russia, alikamatwa nchini Ufaransa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu uhalifu unaohusiana na kushirikisha watoto katika tendo la ngono, na miamala ya ulaghai kwenye mtandao huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akithibitisha rasmi kwa mara ya kwanza kukamatwa kwa Durov tangu alipokuwa anashikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Le Bourget nje ya Paris siku ya Jumamosi jioni, alisema hakukamatwa kwa sababu za kisiasa, licha ya maoni mengi ya uongo mtandaoni.

“Kukamatwa kwa rais wa Telegram kwenye ardhi ya Ufaransa kulifanyika kama sehemu ya uchunguzi wa mahakama unaoendelea,” Macron aliandika kwenye mtandao wa X.

“Huu sio hata kidogo uamuzi wa kisiasa. Ni jukumu la majaji kuamua,” aliongeza.

Katika taarifa iliyofuata, mwendesha mashtaka wa Paris Laure Beccuau alisema Durov alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya mtu ambaye hakutajwa jina ulioanzishwa na kitengo cha uhalifu wa mtandaoni tarehe 8 Julai.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Durov anaweza kuendelea kushikiliwa hadi Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG