Hatua hiyo imechukuliwa baada ya afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki kuishutumu Instagram kwa kuzuia ujumbe wa maombolezo yaliyotolewa kufuatia kuuwawa kwa Ismail Haniyeh, kiongozi wa kikundi cha wanamgambo wa Palestina, Hamas.
Uraloglu alisema Uturuki ilikuwa imeelezea hisia fulani nyeti kuhusu kufuata sheria za Uturuki katika mkutano uliopita uliokuwa na wawakilishi kutoka Instagram wiki iliyopita.
Afisa wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun Jumatano aliikosoa Instagram kwa madai ya “udhibiti, uhalisia na kwa urahisi,” kuhusu kile alichosema uamuzi wake kuzuia ujumbe wa rambi rambi kwa Haniyeh baada ya mauaji yake katika mji mkuu wa Iran, Tehran Julai 31.
Iran na Hamas wameishutumu Israel kwa kufanya mashambulizi yaliyomuua Haniyeh saa kadhaa baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya wa Iran. Israel haijadai kuhusika na shambulizi hilo.
Uturuki ni ya tano duniani katika nchi zinazotumia zaidi Instagram, huku kukiwa na watumiaji milioni 57, ikiifuatia India, Marekani, Brazil na Indonesia, kulingana na data za Statista.
Forum