Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 10:19

Serikali ya uturuki itafanya mazungumzo na maafisa wa mtandao wa Instagram


Logo ya Instagram
Logo ya Instagram

Ni baada ya afisa wa juu wa Uturuki kuishutumu Instagram kwa kuzuia ujumbe wa rambirambi kuhusu mauaji ya Ismail Haniyeh

Serikali ya Uturuki itafanya mazungumzo na maafisa wa Instagram leo Jumatatu baada ya kuzuia fursa ya kuingia katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu, Abdulkadir Uraloglu alisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X.

Hatua hiyo imekuja baada ya afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki kuushutumu mtandao wa Instagram kwa kuzuia ujumbe wa rambirambi kufuatia mauaji ya Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas.

Uraloglu alisema Uturuki imeelezea hisia fulani kuhusu kufuata sheria za Uturuki katika mkutano wa awali na wawakilishi wa Instagram wiki iliyopita.

Afisa wa mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun siku ya Jumatano aliikosoa Instagram kwa madai ya “udhibiti, uhalisia na rahisi,” juu ya kile alichokiita uamuzi wake wa kuzuia ujumbe wa rambirambi kwa Haniyeh baada ya mauaji yake katika mji mkuu wa Iran Tehran hapo Julai 31.

Forum

XS
SM
MD
LG