Rais wa Kenya William Ruto, alisema Ijumaa kwamba hivi karibuni atafanya mabadiliko katika serikali yake, kufuatia wiki kadhaa za maandamano yaliyoanza kama ghadhabu za mitandaoni, kupinga ongezeko la kodi,na ambayo yaligeuka na kuwa ghasia, na hata kupelekea shambulizi kwa bunge la kitaifa.