Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 25, 2024 Local time: 06:00

Mazungumzo ya Gaza yanatafuta njia mbadala ya uwepo wa majeshi ya Israeli mpakani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gabi Ashkenazi, kulia, akikutana na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry (hayuko katika picha), wakati wa mazungumzo ya ngazi ya juu kutafuta suluhu kati ya Israel na kikundi cha wanamgambo wa Hamas katika Kasri ya Tahrir Cairo, Misri,…
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gabi Ashkenazi, kulia, akikutana na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry (hayuko katika picha), wakati wa mazungumzo ya ngazi ya juu kutafuta suluhu kati ya Israel na kikundi cha wanamgambo wa Hamas katika Kasri ya Tahrir Cairo, Misri,…

Wapatanishi wa sitisho la mapigano wa Israeli na Misri wako katika mazungumzo kuhusu mfumo wa kielekrotiniki wa ulinzi wa mpakani kati ya Gaza na Misri ambao unaweza kuiruhusu  Israel kuwarudisha nyuma wanajeshi wake iwapo sitisho la mapigano litakubaliwa.

Taarifa hiyo ni kulingana na vyanzo viwili vya Misri na chanzo cha tatu ambacho kinafahamu vizuri suala hilo.

Swali iwapo majeshi ya Israeli yabakie mpakani ni moja ya masuala yanayo zuia uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa sababu pande zote kikundi cha wanamgambo wa Palestina Hamas na Misri, mpatanishi katika mazungumzo hayo, wanapinga Israel kuendelea kuweka majeshi yake huko.

Israel ina wasiwasi kuwa iwapo wanajeshi wake wataondoka eneo la mpakani, linalotambuliwa na Israel kama kivuko cha Philadelphi, kitengo cha silaha cha Hamas kinaweza kupitisha kwa magendo silaha na bidhaa kutoka Misri kuingia Gaza kupitia mahandaki ambayo yatawaruhusu kujenga tena uwezo wao wa silaha na kuitishia tena Israel.

Mfumo wa ulinzi wa kielektroniki, iwapo pande katika mashauriano zitakubaliana kuhusu maelezo, hivyo inaweza kurahisisha kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano- japakuwa bado kuna vikwazo vingine vya kutatuliwa.

Majadiliano kuhusu mfumo wa ulinzi wa mpakani uliripotiwa siku za nyuma, lakini Reuters inaripoti kuwa kwa mara ya kwanza Israel inajihusisha na mazungumzo hayo ikiwa ni sehemu ya duru ya sasa ya mazungumzo, wakiwa na fikra ya kurudisha nyuma majeshi yao kutoka katika eneo la mpakani.

Chanzo ambacho kinafahamu vyema suala hilo, ambacho kilizungumza katika misingi ya kutotajwa, kilisema mazungumzo hayo “ kimsingi uwekaji wa sensa zitakazo jengwa upande wa Misri wa kivuko hicho cha Philadelphi.

Forum

XS
SM
MD
LG