Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:55

Majeshi ya Israeli yasambaza vipeperushi, Wapalestina wakabiliwa na hofu kubwa


Wapalestina, waliokimbia kutoka mashariki ya mji wa Gaza City baada ya kutolewa amri na jeshi la Israeli kutoka maeneo jirani, wakibeba mizigo yao, katika vita vya Israel-Hamas huko Gaza City.
Wapalestina, waliokimbia kutoka mashariki ya mji wa Gaza City baada ya kutolewa amri na jeshi la Israeli kutoka maeneo jirani, wakibeba mizigo yao, katika vita vya Israel-Hamas huko Gaza City.

Familia za Wapalestina waliokoseshwa makazi zilionekana zikikimbia mji wa Gaza, wakielekea kusini mwa Ukanda wa Gaza Alhamisi (Julai 11), kufuatia amri ya hivi karibuni ya Israeli ikiwataka waondoke eneo hilo.

Majeshi ya Israeli yalidondosha vipeperushi vikiwataka wakaazi waondoke ambapo safari yao ya kuhama iliwapeleka hadi Salah al-Din huko wilaya ya Al-Nuseirat kusini mwa Gaza.

“Tunaelekea huko Deir Al-Balah. Bila shaka hatukuweza kulala usiku kucha kutokana na mashambulizi, hofu na wasiwasi,” alisema Aisha Kazat, ambaye alionekana akikimbia eneo hilo na familia yake.

Watu walionekana wakichukua kile walichoweza, ikiwemo farasi, katika magari aina ya pick up wakielekea kusini mwa Gaza.

“Tunashuhudia mambo mengi. Wanajeshi wengi wametusimamisha na kutupekua na wametuweka kwa muda wa saa nzima. Ni adhabu… siwezi hata kuzungumza. Tuna hali ngumu kuweza kuielezea au kuzungumzia,” alisema Mona Al-Husseini alisema Mpalestina aliyekimbia.

Wanamgambo wa Hamas wanasema shambulizi kali litakalofanywa na Israeli katika mji wa Gaza City wiki hii litaharibu juhudi na hatimaye kumaliza vita wakati tu mazungumzo hayo yameingia hatua ya mwisho.

Forum

XS
SM
MD
LG