Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 02, 2024 Local time: 07:45

Jeshi la Israel lanasa silaha zinazoaminika kutoka Lebanon


Ndege ya vita ya Israel ikiwa kwenye anga ya mapaka kati ya Israel na Lebanon July 3, 2024.
Ndege ya vita ya Israel ikiwa kwenye anga ya mapaka kati ya Israel na Lebanon July 3, 2024.

Jeshi la Israel Alhamisi limefanya mashambulizi kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, wakilenga kile walichosema ni wanamgambo waliorusha roketi kutoka mji huo.

Jeshi hilo la IDF limeongeza kusema kuwa limeingilia kati takriban roketi 5 zilizorushwa kutoka Rafah. Vikosi vya Israel pia vimenasa silaha zinazoshukiwa kuwa za anga, zilizovuka kutoka kusini mwa Lebanon, mapema leo, wakati droni zilizokuwa zimeandamana nazo zikitunguliwa pia kwenye eneo la Israel la Galilayo.

Wapiganaji wa Hebollah kutoka Lebanon wamekuwa wakishambuliana kwenye mpaka tangu vita vya Gaza vilipoanza, na kuzua hofu ya mapigano hayo kusambaa kieneo. Mapigano pia yameripotiwa kuendelea leo mjini Gaza City, kaskazini mwa Gaza, siku moja baada ya Israel kutoa ilani kwa wakazi kuondoka kwa ajili ya usalama wao.

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema Jumatano kwamba kuondoka kwa wakazi kutaongeza mateso ya familia za kipalestina, nyingi zikiwa zimehama kwa zaidi ya mara moja. Shirika la Chakula Duniani, WFP, Jumatano kupitia ukurasa wa X limesema kuwa kumekuwa na ongezeko la shuguli za kijeshi huko Gaza City, suala ambalo limeongeza mahitaji ya misaada ya kibinadamu, likiongeza kuwa hali iliopo ni hatari na isiyoweza kutabirika.

Forum

XS
SM
MD
LG