Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:47

Shambulizi la Israel limeua kamanda wa Hezbollah


moshi kutokana na shambulizi la Israel katika kijiji cha Shihin kusini mwa Lebanon karibu na mpaka na Israel.June 28, 2024. AFP
moshi kutokana na shambulizi la Israel katika kijiji cha Shihin kusini mwa Lebanon karibu na mpaka na Israel.June 28, 2024. AFP

Shambulizi la Israel limemuua kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo wa Hezbollah, kusini mwa Lebanon, wakati mivutano kati ya pande hizo mbili ikiendelea kuongezeka.

Shambulizi hilo la anga karibu na mji wa pwani wa Tyre limetokea wakati kuna ongezeko la juhudi za kimataifa za kidiplomasia, kuzuia mgogoro kati ya Hezbollah na jeshi la Israel kuongezeka na kuwa vita ambavyo vinaweza kusababisha mgogoro wa moja kwa moja kati ya Israel na Iran.

Taarifa ya Hezbollah imemtaja kamanda aliyeuawa kuwa Mohammad Naameh Nasser, anayejulikana kwa jina Abu Naameh.

Naameh ni afisa wa juu sana wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, kuuawa tangu kifo cha Taleb Sami Abdullah, aliyeuawa katika shambulizi la anga la Juni 11.

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, amemtaja Abdullah kuwa mtu muhimu katika kundi hilo tangu mapambano yalipoanza Oktoba 8, akiongoza kikundi cha Nasr.

Forum

XS
SM
MD
LG