Vifaru vya Israel vimewekwa katika mpaka wake na Gaza mapema Jumapili asubuhi. Huku moshi ukizidi kutanda kutoka kwenye majivu ya shambulizi jingine la kijeshi.
Siku moja tu iliyopita, Katikati mwa Ukanda wa Gaza mashambulizi ya anga ya Israel yameua Wapalestina watatu kwa mujibu Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.
Mwandishi wa habari wa Associated Press kwenye eneo amethibitisha kuona maiti za miili mitatu ya watu.
Kwa mujibu wa idadi rasmi ya wizara hiyo idadi ya vifo upande wa kaskazini imefikia Wapalestina 37,800 tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi makali kufuatia mashambulizi ya Oktoba saba.
Ilikuwa wakati huo ambapo Hamas na washirika wake walivamia ndani ya Israel na kuu takriban raia 1,200 na kuwateka nyara wengine 250.
Israel imeapa kuwatokomeza Hamas kwa gharama yoyote ile na kuwarejesha mateka ambao walichukuliwa siku hiyo.
Katika mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alielezea kile alichokiita “kazi muhimu ni kuwaachia huru mateka,” pia uchelewesho kwa makubaliano ya amani.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel anaeleza: “Kila mtu anafahamu ukweli. Hamas ndiyo kikwazo pekee katika kuachiliwa kwa mateka wetu. Kukiwa na mchanganyiko wa hisia na shinikizo la kisiasa na kijeshi – juu ya yote hayo, shinikizo la kijeshi -- tutawarejesha wote hao. Mateka wetu wote 120. Walio hai na waliokufa.”
Lakini kwa Waisrael wengi, hiyo pekee haitoshi. Wakati maelfu wakiwa wamekusanyika tena mjini Tel Aviv wakitaka uchaguzi ufanyike kumuondoa Netanyahu huku kukiwa na wito wa hatua kubwa kuchukuliwa kuwarejesha mateka waliochukuliwa Oktoba saba.
Marekani, pamoja na washirika wa kikanda, wamekuwa wakifanya kazi kusimamia makubaliano ya amani kati ya Israel na Hamas.
Lakini inaonekana kuwa pande zote zimejikita, wakati Hamas ikidai sitisho kamili la mapigano na Israel iondoke kabisa kutoka Gaza. Wakati Israel inakubali sitisho la muda tu mpaka Hamas haipo tena.
Osama Hamdan, Afisa Mwandamizi, Hamas anasema: “Hakuna maendeleo ya kweli yaliyopatikana katika kumaliza mapigano…Kwa mara nyingine tena, Hamas iko tayari kwa makublaiano chanya kwa pendekezo lolote ambalo litafanikisha sitisho la kudumu la mapigano, kuondoka kabisa kutoka Ukanda wa Gaza na makubaliano ya kubadilishana watu.”
Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema vita vimewakosesha makazi takriban wakazi milioni 2.3, ambao hivi sasa wanaisha katika mahema miji huku viwango vya joto vikiwa juu mno zaidi ya digrii 32 celcius.
Marekani, kwa upande wake, bado ni mshirika mkuu wa vifaa na fedha wa Israel, lakini wito wa sitisho la mapigano uaongezeka kila siku huku picha zikimiminika za idadi ya vifo vya raia katika vita.
Mpaka ilipofika Ijumaa, Umoja wa Mataifa umesema watu elfu 60 wamelazimika kukimbia maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Gaza City.
Balozi wa Marekani nchini Misri, Herro Mustafa Garg, alitembelea ghala ya bidhaa huko Sinai Kaskazini na kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah huku kukiwa na wito wa karibuni kwa amani.
Forum